Mark 5:21-26

21 aIsa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu ukamzunguka yeye akiwa hapo kando ya bahari. 22 bKisha mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake, 23 cakamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye atakuwa hai.” 24Hivyo Isa akaenda pamoja naye.

Umati mkubwa wa watu ukamfuata, nao watu wakawa wanamsonga.
25 dHapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili. 26Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya.
Copyright information for SwhKC